wakaaji wa Luhololo waomba msaada warudi kwao

village de Luhololo

Luhololo, Uvira tarehe 10-05-2015
Mwaka mzima sasa wakaaji wa kijiji cha Luhololo walihama maskani
 yao. Luhololo ni kijiji chenye kupatikana umbali  wa ma saa mawili ya mwendo wakutembea na  miguu, eneo ya magaribi mwa Kahwizi, nyanja za kati tarafani Uvira wilayani Muhungu .
Wakaaji hao walikimbia tangu
 machi mwaka wa 2014, kutokana na wizi pia ubakaji uliokua unatekelezw na majambazi wenye silaha wasiojulikana. Hadi sasa hata wapita njia wanahofia kupita eneo hilo kwa vile wahalifu wanazidi kuendesha hujuma zao, baadhi yao wanajificha ndani ya mabako ya nyumba
zilizoachwa.
Muasirika mmoja  alieficha jina lake alieleza kwamba
 wanaomba wakuu viongozi kujitahidi kurudisha usalama eneo hilo, duru hio ilisema tena kuwa wahamiaji wanaishi katika hali mbaya, na wana
haja ya kurudi kwao, ila wanahofia hali ya usalama mdogoilioko. Wakati
huohuo, wanaomba serkali na mashirika ya kiutu  kuwasaidia.

UviraOnline

One Comment on “wakaaji wa Luhololo waomba msaada warudi kwao”

  1. i am so happy to see a website like this which help us to get more information about our city. May God bless you

Comments are closed.