Uvira-RDC: Kamanda wa operesheni sukula ya pili, kufurahishwa na mbinu za kuwaweka karibu askari jeshi na raia

comandant-Bwange-Safari-GustaveKamanda wa sekta ya operesheni sukula ya pili kusini mwa jimbo ya kivu ya kusini  jijini Uvira ,ataja kufurahishwa na mbinu za kuwaweka karibu askari jeshi na raia.

Jemadari Bwange Safari Gustave alijulisha hayo baada ya mchezo wa kandanda uliozikutanisha siku ya kwanza jioni, Timu ya askari jeshi na wakaaji wa Uvira, mechi ilochezeka kwenye uwanja wa umoja. Michezo hiyo imetukia katika mradi uitwao amani, ya shirika search for common ground centre lokole ,na serkali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo.
Kwa upande wake jemadari  wa operesheni Sukula ya pili kusini mwa jimbo ya kivu ya kusini,alisema askari jeshi wako kwa ajili ya raia, kwa hio jambo la kuwakusanya pamoja ni muhimu,ili kuleta mariziano na
kuchangia kwa usalamawa eneo hili.Jemadari wa jeshi la taifa FARDC, alisema pia kwamba mbinu zingine za kuwakusanya pamoja raia na askari jeshi zitaandaliwa kwa kushirikiana na kufanya kazi za pamoja
kwa usafi wa mji iitwayo salongo.

Utafahamu kwamba mechi kati ya askari jeshi na raia ilikomeshwa kwa kufungana bao moja kwa moja. Operesheni sukula ya pili kusini mwa jimbo ya kivu ya kusini, ni katika lengo ya majeshi ya taifa kutokomeza vikundi vinavyo shikilia silaha vya wakongomani na vya kigeni.


 

UviraOnline: Mazambi M’penge