Mulongwe, maisha ya arehemu Maria LUBULA NGALOLERA.

Mulongwe, Tarehe 30 /12/2016 MAISHA YA MAREHEMU KIINGILIO :

Mwanaadamu aliyezaliwa na mwanamuke siku zake za kuishi si nyingi nazo hujaa taabu, Ayubu 14 :1 KUZALIWA : Marehemu alizaliwa pa Kabondola, Groupement ya Muhungu, tarehe …… / ….. / 1919

MAJINA : Marehemu alipozaliwa, alipewa majina yafwatayo : Maria LUBULA NGALOLERA, wa Jamaa la Banyakatanda. WAZAZI : Baba yake aliitwa Kamete wa Jamaa la Banyakatanda, naye ni Marehemu. Mama yake aliitwa Eva wa Jamaa la Batumba, naye ni marehemu.

MASOMO : Marehemu hakujaliwa kusoma.

WOKOVU : Marehemu Maria alimpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yake na kubatizwa katika maji mengi wakati wa Wamisionary

BECMAN. KAZI : Marehemu Maria, alijishuhulisha saana na Kazi za Kilimo na biashara ndogondogo.

NDOA : Marehemu Maria, alifunga pingu za Maisha mwaka wa 1939 ; na Mume wake aliyekuwa anaitwa kwa jina la Jospeh ALIMASI wa Jamaa la Balizi. Naye ni Marehemu.

UZAZI : Marehemu Maria, alijaliwa na Mwenyezi Mungu kuzaa watoto Wanne. Mukiwemo watoto Wakiume Wawili (2) na Watoto wakike wawili (2). Watoto wote wane wako hai.

MAGONJWA : Marehemu Maria alisumbuliwa saana na Ugonjwa wa Moyo tangu mwaka wa 2011. Alitunzwa kwenye ma Hospitali na ma Zainati mbalimbali ila haikufua dafu. Ilipofika siku ya tano (Ijumaa), tarehe 30/12/2016 na saa moja za asubui, Maria LUBULA NGALOLERA akaiaga dunia.

MWISHO : Marehemu Maria Lubula aliishi hapa duniani miaka 97 na kuacha Watoto 4, Wajukuu 24, Wajukuluza 27 na Kajukuluza 1. Wote kwa jumla ni jamaa la watu 56. Jamaa la Balizi, Banyakatanda, Kanisa na Marafiki pia na Majirani, tunamtakia mapumziko mema.

AHSANTE


UO: Aubain Mwaka