Uvira: kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu CICR, yaombwa kurudilia operesheni ya kuorozesha upya waasirika.

Mjini uvira jimboni kivu ya kusini, baadhi ya waasirika wa mafuriko waishio kwenye mitaa mingi ya kata ya kakombe, kibondwe, kasenga na mulongwe, wanaomba kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu CICR, kurudilia operesheni ya kuorozesha upya waasirika.

Siku ya tatu meyi 27, mbele ya saa sita mchana,watumishi wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu waliokua wanaorozesha waasirika, wengi hawakumaliza kazi hiyo vizuri, kwa vile raïa wengi walikua wanawafuata nyuma.

Wanao jiita waasirika wa kweli wakiwa wenye kupokelewa na jamaa yao ya karibu, waliomba kwamba kazi ya kuorozesha waasirika irudiliwe upya na mbele ya kuifanya wahamasishe kwanza wakaaji wote.

Shirika mpya ya kiraia “nouvelle société civile congolaise NSCC, yataja kuwa na wasiwasi na hali hiyo, Ila wanatarajia kuonana na wakuu viongozi wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu CICR ya Uvira, kwa kupata suluhisho.

Mkuu kiongozi aliekua anasimamia watumishi wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu eneo ya kata ya kakombe, alieleza wakaaji kwamba licha ya kubaki na fomu ima jetons nyingi mkononi, wamekomesha kazi, ila wanaweza kurudi kuorozesha waasirika kama wakuu viongozi wao watawaruhusu.


Mazambi WakuLitete