Tanzania-RDC: Mizigo yote ya DRC itapitia Bandari ya Dar. Tulisitisha sababu ya urasimu na upotevu

kabila-magufuli-tanzaniaRais Joseph Kabange Kabila amekuwa na mazungumzo na Rais Magufuli kabla ya kukutana na waandishi wa habari Ikulu Dsm leo.Katika mambo waliyoongea na kuwashirikisha waandishi wa habari ni ushirikiano wa kibiashara,ulinzi na Usalama pamoja na ujirani mwema.

Rais Kabila anasema baada ya maongezi na Rais JPM amejiridhisha sasa kuwa bandari ya Dsm ni salama na ataanza tena kupitisha mizigo yote ya DRC ktk bandari hii,ambayo kwa kipindi fulani walisitisha na kuanza kutumia kwingine kutokana na kodi,urasimu na upotevu wa mizigo.Katika mazungumzo ya leo,Serikali ya Tz imemuhakikishia Rais Kabila kuwa mizigo yote ya DRC itakuwa na “Grace period” ya siku 14 hadi 30 bandarini.

Pia Rais Kabila anasema wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kupunguza vituo vya ukaguzi wa mizigo itakayokuwa inatoka bandarini kwenda Congo DR,hali hii ya kupunguza vituo vya ukaguzi itarahisisha wafanyabiashara kufikisha mizigo kwa wakati na kupunguza ghalama za usafirishaji.Rais Kabila pia amemuahidi Rais JPM mara afikapo DRC atahakikisha anafanya mabadiliko makubwa ktk Mamlaka ya Kodi ya DRC ambayo imekuwa ikalalamikiwa na wafanyabiashara wengi kutokana na urasimu na ukiritimba unaokuwa kama kikwazo ktk maendeleo ya biashara.

Rais Kabila pia amezungumzia suala la amani mashariki mwa DRC,na kusema hali si kama inavyolipotiwa na vyomba vya habari vya nje,japo kuna vikundi vichache vya uasi vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao.Amerishukuru JWTZ chini ya Umoja wa Mataifa kuendelea kutunza amani ya DRC.

Naye Rais Magufuli alianza kwa kumwambia Rais Kabila “Kuonesha kuwa Tanzania na DRC tuna uhusiano Mzuri nimemwambia Rais Kabila kuwa Watanzania wengi wanapenda Miziki ya Zaire“.

kabila-magufuli-tanzania_2

Pia Rais Magufuli ameendelea kumuhakikishia Rais Kabila kumpa ushirikiano wa kiulinzi kwa kuwakutanisha viongozi wa vyombo vya ulinza na usalama vya DRC na Tanzania.Rais Magufuli kamshukuru Kabila kurudisha nia yake ya kutumia bandari ya Dsm kwa kupitisha mizigo yake.

Rais Magufuli ameongelea kuwa wamegusia suala la uchaguzi wa DRC ambapo Kabila amemwambia amelipeleka mbele ili kuhakikisha watu wote wanapiga kura,kwani miaka mitano iliyopita kulikuwa na wapiga kura milioni 35 na sasa ni milioni 45,hivyo wanahitaji muda ili kujumuisha wapiga kura wengi ambao wengi wao ni vijana.

Rais Magufuli amewataka raia wote wa DRC walioko kwenye makambi ya wakimbizi Tz,kurudi DRC kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi watakaorudisha amani ya nchi yao na kwafanya wao wasiwe wakimbizi ktk nchi za watu.

Katika ziara hii,Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na DRC wametiliana sahihi mkataba wa kutafuta mafuta ktk eneo la ziwa Tanganyika.Upatakinaji wa mafuta hayo na hatimaye kuchimbwa utaleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Baada ya kuongea na waandishi wa Habari,mchana wa saa nane wataweka jiwe la msingi Bandari ya Dsm na baadae kuwa na dhifa ya kitaifa Ikulu-Dsm


JamiiForums article du 04 octobre 2016