Wakaaji wa mji wa Uvira, baada ya kukabiliwa na wooga wa wezi, wizi na ubakaji kwa siku nyingi, wamebahatika kusherehekea sikukuu ya Noeli katika hali ya utulivu. Viongozi wa serikali wameahidi kuchunga ulinzi wakati huu wa sikuu kubwa.
Tarehe 24 desemba, makanisa mengi yamebatiza watu kwenye maji mengi ya Bahari ya Tanganyika. Kanisa la 8e CEPAC MULONGWE imebatiza watu 151 walioamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Siku ya 25 desemba, makanisa mengi yamekumbuka kuzaliwa kwake Yesu, nyimbo nyingi zimeimbwa na mafundisho yenye maana saana. Siku ya jumapili, tarehe 27 desemba, mikutano ya injili iliandaliwa barabarani. Watu wengi pia wameamini Yesu Kristo.
Sikukuu ya Noeli imepitika katika utulivu hapa Uvira.
Pour Uviraonline : Aubain Alan Popov MWAKA MIGAN