Karibu katika kipindi cha leo tarehe 08 Januari 2016.
1. POSTA: kituo cha kutuma ao kupokea barua ao mizigo.
2. TARISHI: mtu anaekuwa kwenye posta akiwa na kazi ya kugawa barua kwa wenyeji,kwa kifaransa ni facteur.
3. MKONGOJO; mti ao chuma kinachomsaidia mzee ao mlemavu kutembelea,kwa kifaransa ni bequille.
4. KOMBA(MAKOMBA wingi); mnyama mdogo mwenye macho makubwa anaependa kulialia usiku,kwa kifaransa ni kalago.
5. SEREDANI; chombo cha jikoni kinachotumia mkaa kwa kupikia chakula,hapa chombo kinajulikana kama mbabula, kwa kifaransa ni brazero.
6. MSEJA; karatasi inayotumika kwa kulainisha mbao ao chuma,kwa kingereza ni sand paper.
7. DIWANI; mkuu wa mji,maire kwa kifaransa na mayor kwa kingereza.
8. SANDUKU LA POSTA; anwani inayotumiwa kupitishia barua,kwa kingereza ni postal address.
9. IBUKA; ni kutoka kwa ghafla ndani ya maji.
10. INJINI; mtambo unaotoa nguvu kea kuendesha chombo,kwa kifaransa ni moteur.
Mwisho wa kipindi.