Luhololo, Uvira tarehe 10-05-2015
Mwaka mzima sasa wakaaji wa kijiji cha Luhololo walihama maskani yao. Luhololo ni kijiji chenye kupatikana umbali wa ma saa mawili ya mwendo wakutembea na miguu, eneo ya magaribi mwa Kahwizi, nyanja za kati tarafani Uvira wilayani Muhungu .
Wakaaji hao walikimbia tangu machi mwaka wa 2014, kutokana na wizi pia ubakaji uliokua unatekelezw na majambazi wenye silaha wasiojulikana. Hadi sasa hata wapita njia wanahofia kupita eneo hilo kwa vile wahalifu wanazidi kuendesha hujuma zao, baadhi yao wanajificha ndani ya mabako ya nyumba
zilizoachwa.
Muasirika mmoja alieficha jina lake alieleza kwamba wanaomba wakuu viongozi kujitahidi kurudisha usalama eneo hilo, duru hio ilisema tena kuwa wahamiaji wanaishi katika hali mbaya, na wana
haja ya kurudi kwao, ila wanahofia hali ya usalama mdogoilioko. Wakati
huohuo, wanaomba serkali na mashirika ya kiutu kuwasaidia.
UviraOnline
i am so happy to see a website like this which help us to get more information about our city. May God bless you