Karibuni Kwenye kipindi cha leo tarehe 22 januari 2016.
1. MABANO YA MRABA; alama zinazotumika kwa kufungia kitenzi,parenthèse kwa kifaransa.
2. DOBI; mtu anayefua ao kupiga pasi nguo kwa kulipwa pes.
3. SIAGI; mafuta yanayopakwa kwenye mkate ao kupikia keki ao vyakula vingine, butter kwa kiingereza.
4. SAJINI; askari mwenye cheo daraja moja zaidi kuliko koplo,sergeant kwa kiingereza.
5. MSHUMAA (MISHUMAA wingi); kifaa kilichotengenezwa na nta iliyogandihwa na utambi katikati ili kumulika unapowashwa, bougie kwa kifaransa.
6. NTA; kitu kigumu kama gundi kinachotengenezwa na nyuki, wax kwa kiingereza.
7. GUNDI; majimaji yanayonata na kutumiwa kwa kushikanisha vitu, glue kwa kiingereza.
8. ZAHANATI; (MAZAHANATI Wingi); hospitali ndogo yenye kutoa matibabu kwa magonjwa madogomadogo, dispansaire kwa kifaransa.
9. CHACHAWIZO (MACHACHAWIZO wingi}; hali ya kuto kuwa na imani. Unga wenye mbegu ya kiume ulio ndani ya ua, pollen kwa kiingereza.