DARASA LA KISWAHILI: Tarehe 15 Januari 2016

Karibu kwenye kipindi cha leo tarehe 15 Januari 2016.

1. TARAKILISHI; ni mashine inayopokea habari na kuishughulika kulingana na ratiba yake,ordinateur kwa kifaransa ao computer kwa kiingereza.

2. PUKU; ni kifaa chenye vitufe viwili cha kuingizia data kwenye tarakilishi,souris kwa kifaransa.

3. GLOPU; kitufe kidogo chenye umbo la mviringo mfano wa yai kilichotengenezwa kwa kioo ili kutoa mwangaza wa umeme,kwa kifaransa ni empoule ao bulb kwa kiingereza.

4. TASLIMU; tendo la kununua kitu kwa kutoa pesa bila kubaki na deni,mfano;nimenunua kwa pesa taslimu dala mia,yaani sikubaki na deni.

5. KAMPENI; shughuli inayofanyika ili kuwavutia watu,campagne kwa kifaransa.

6. KAMPUNI; shirika la kufanyia biashara ao kazi zingine,company kwa kiingereza.

7. KANCHIRI; nguo inayovaliwa na wanawake kwa kushikilia matiti,soutien~gorge kwa kifaransa.

8. TITI(MATITI wingi); sehemu iliyo kifuani kwa mwanamke itoayo maziwa kama chakula kwa mtoto mchanga,sains kwa kifaransa.

Mwisho wa kipindi.


Darasa-la-kiswahili

Leave a Reply