Karibuni katika kipindi cha leo tarehe 01 januari 2016.
1. JAHAZI: ni chombo cha usafiri majini kilichofunikwa juu kwa kitambaa.
2. ABIRI: ni kujipakiza ndani ya chombo cha usafiri, mfano; hivi sasa ninaabiri ndani ya ndege ili kuja uvira.
3. ABIRIA: mtu anayepatikana ndani ya chombo cha usafiri,passager kwa kifaransa.
4. CHOTARA: mtoto aliepatikana kutokana na wazazi wenye rangi mbili,mfano; rais barack obama ni chotara kwa kuwa baba yake ni mjaluo wa kenya na mamae ni mtu wa ulaya,mulâtre kwa kifaransa.
5. FAKACHI ao FITNA: ni tabia ya mtu kusema mambo ya watu wengine ili kuwachochea,comérage kwa kifaransa.
6. RABA: viatu vyenye soli ya mpira.
7. SOLI: Sehemu ya chini ya kiatu unayotumia kwa kukanyagia unapotembea.
8. MZEE: Mtu mwenye umri mkubwa.
9. AJUZA (MAAJUZA wingi): Ni mzee wa kike.
10. SHAIBU: Mzee wa kiume.
Mwisho wa kipindi.