Uvira-RDC: Kumbukumbu ya miaka 498 ya kanisa la kiluteri ERLC

Kumbukumbu ya miaka 498 ya matengenezo ya kanisa la kikristu ilisherehekewa siku ya Mungu novemba mosi jijini Uvira,  kwenye kanisa la matengenezo ya kiluteri inchini Congo ya kidemokrasia, kwenye kata ya nyamianda .

la bible en afriqueKwake kiongozi na mwakilishi wa kanisa la kiluteri ERLC, siku hio ina umuhimu kwa makanisa yote ya kiprotestanti. Kwa sababu ni hayo ndio imetiya misingi ya matengenezo ilio letwa naye Martin Luther, alieleza hivin mchungaji Edouard ILUNGA MUTOMBO. Kwa hio ni jambo la ukweli kwa mkristu yeyote kuzingatia neno la Mungu, kuliko sheria za wanadamu ambazo haziwezi kumuokoa mtu.

Alifundisha kupitia andiko la Zaburi 40;1-8. Kiongozi huyowa kanisa la ERLC alitowa mwito kwao wakristu kutia tumaini yao kwake Mungu pekee ili matengenezo yakamilike.

Utajua kwamba ni tangu mwaka wa 2014 ndipo kanisa la matengenezo ya kikristu la kiluteri yaendesha shuruli zake inchin Congo baada ya kujiondoa kwa kanisa la asili.


 

Pour UviraOnline: Mazambi M’penge Wakul’itete