Baraka-RDC: Ungondjwa wa maleria unazuka kwa kiasi kubwa Baraka

Hopital ya BarakaUngondjwa wa maleria unaripotiwa kuzuka kwa kiasi kubwa sana pa Baraka katika hopital kuu na katika vituo vinavyo zaminiwa na shirika la MSF / Hollande tarafini Fizi. Watu zaidi ya 300 wanapimwa maleria kwa siku.

Kulingana na docteur IBUCWA NYAMANGYOKU Joseph, mganga mkuu wa hopital ya Baraka, mwaka huu ni kama mwaka uliyopita, ila akuripotiwi vifo vingi mwaka huu bali ni upungufu kali wa damu mwilini.

Hopital kuu la Baraka na wazamini wao shirika la MSF / Hollande, walisema mbu apatikanaye kando ya nyumba ndiye anasababisha kuzuka kwa ungondjwa, kumbe nivema watu kusafisha vema mazingira, kulala usiku muzima ndani ya chandaruwa yenye kuwekwa dawa pamoja na kujielekeza kupimwa pale tu unapo sikiya dalili za maleria kwenye kituo cha afya cha karibu.

Docteur IBUCWA NYAMANGYOKU Joseph, aliomba piya watu kujitoleya kwa kupana damu ili kuokowa maisha ya watu wengine.


Source: Umoja Baraka