MSANII MAARUFU MUZALENDO , AZUNGUMZIA KAZI YAKE

swagg

Kwa mara ya kwanza, Umoja radio kutoka nchini Uholanzi inakuletea story ya msanii wa kizazi kipya kwa jina aliyopewa na wazazi wake anajulikana kama Djuma, lakini kikazi anajulikana kwa jina la Sean wa Sean, Muzalendo, Super Mario, kutoka Uvira, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alianza kazi ya muziki hasa uhimbaji pa Uvira tangu mwaka wa 2006, katika kundi lihitwalo ” Watu kasi Halisi” D.R.Congo. Kiufupi ni msanii wa muda wa kutosha kwenye gemu hiyo. Tukizungumza naye kwenye mtandao wa kijamii wa facebook, staa huyo alisema kwamba, hadi sasa ametoa nyimbo tano ambazo zinaenda kwa majina haya yafuatayo: Tupeni Haki, Wendo wangu feat Olga (Buja Record), Uko Wapi, Maman ni Maman, Message. Hiyo ndiyo orodha ya nyimbo ambazo ameshazitoa.

IMG_37042542171559

Wimbo huu wa mwisho ” Message” umekokota hisia za watu kwa maneno muhimu yanayopatikana ndani, hata namna ya kurapu inafurahisha sana. Hapo chini unaweza kusikiliza na kuona video ya wimbo huo.

Uimbaji wa Muzalendo unahusiana na kuelimisha jamii. Pamoja na kuelimisha jamii, Muzalendo anapendelea kuwa msanii wakimataifa na baada ya kufanikisha kwenye gemu ya muziki, ataitaji pia kuwasaidia wale wasiojiweza, vile vile na kuwasaidia wasanii wenzake ambao watakaohitaji kujulikana kama yeye.

Pamoja na hayo, Umoja radio imefurahiya kipaji alichonacho Muzalendo, kufuatana na hayo Umoja radio itakuwa bega kwa bega na msanii huyu kwa kila hatua ya kimziki kwa ajili ya kutangaza kazi zake.

14724_421209694722764_7536554041064944605_n

Ijapo msanii huyu anajulikana kiasi hapo DRC bado haijatosha kwa sababu wengine wamemjua leo baada ya kusoma story yake. Muziki bila mashabiki ni kama shoka bila mpini. Unaweza kutoa sapoti kwa kujulisha rafiki kwamba kuna msaani mwingine anayefanya vizuri katika anga la muziki, pia ushauri, maoni ni sapoti kubwa. Mwisho ni sapoti ya pesa sababu itamuwezesha kutengeneza video, wimbo kubaki kwenye audio haujakamilika. Asanteni kwa kumsapoti kijana wenu Muzalendo a.k.a Sean wa Sean a.k.a Super Mario.

Tizama na kusikiliza wimbo wake MESSAGE hapa chini
Publier par umojaradiongg@gmail.com | 14 March 2015

2 Comments - Write a Comment

Comments are closed.