Montréal-Canada: Cooperative swahili du Canada, huundwa.

Siku ya inn le 15 october waswahili kutoka inchi mbali mbali, walikutana hapa Montreal – Canada, ili yakuzungumuza kuhusia uundaji wa cooperative ya waswahili. UviraOnline alikutana na mumoja wao.

Uvira_Fizi_IMG-20151016-WA0001WILLIAM MUYUKU: ni nini cooperative swahili du canada
SHEMU FALINGO: Cooperative kwa Kiswahili ni: KUSHIRIKIANA.

 WILLIAM MUYUKU: kwanini mumeiunda shirika hili (coperative) hii, lengo lake
SHEMU FALINGO: Tumeunda shirika  hii kwa sababu ya kuona wana inchi wanao sema Lugha hii ya Kiswahili wanaendeleya na kuongezeka hapa Montreal-Canada. Na hasa zaidi kwa sababu ya mambo haya matatu:
1) Kupata nyumba za pamoja 2) Kuendeleza mazoezi yetu ya chakula cha Africa  2) Kupata matibabu katika Lugha yetu ya Kiswahili. 3) Kuchunga Asili zetu, na Lugha yetu ya Kiswahili.

 WILLIAM MUYUKU: hili ni wazo la nani
SHEMU FALINGO: Wazo hili limetolewa na mimi SHEMU FALINGO RUSOMEKA, ambaye ni Muchungaji wa Kanisa la wazalendo wasemao Lugha hii tukufu la Kiswahili, huku akiwashirikisha na viongozi wa wana inchi wasemao Lugha hii ya Kiswahili hapa Canada.

 WILLIAM MUYUKU: Mumeongea nini mu mukutano waleo
SHEMU FALINGO: Mukutano wetu wa Leo: Tulizungumuziya uundaji wa Kama, Uundaji wa kamati na kuweka ma commissioners watakao husika na ma documents.

WILLIAM MUYUKU: ni wanani walio wa member, na kila mtu anaweza kua member
SHEMU FALINGO: Wanambe: Kila anaye sema Lugha ya Kiswahili, akiwa ametoka Africa ao Muzungu ni mwana-Memba.

WILLIAM MUYUKU: neno la mwisho kwako kama president
SHEMU FALINGO: Tuna penda kuwajulisha wana inchi wote wanao sema Lugha ya Kiswahili hapa Canada. Ya kwamba kumeundwa Shirika la wasema Kiswahili limekwisha undwa. Na Shirika hilo limeundwa na wana Inchi kutoka katika inchi hizi zifuatazo: Dem. Rep. ya Congo, 
Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Malawi na Uganda.
Mwenyezi abariki wazo hili.

Asante

Uvira_Fizi_IMG-20151016-WA0017Uvira_Fizi_IMG-20151016-WA0022Uvira_Fizi_IMG-20151016-WA0018Uvira_Fizi_IMG-20151016-WA0001