DARASA LA KISWAHILI: Tarehe 01 januari 2016

Karibuni katika kipindi cha leo tarehe 01 januari 2016.

1. JAHAZI: ni chombo cha usafiri majini kilichofunikwa juu kwa kitambaa.

2. ABIRI: ni kujipakiza ndani ya chombo cha usafiri, mfano; hivi sasa ninaabiri ndani ya ndege ili kuja uvira.

3. ABIRIA: mtu anayepatikana ndani ya chombo cha usafiri,passager kwa kifaransa.

Obanma ni chotara4. CHOTARA: mtoto aliepatikana kutokana na wazazi wenye rangi mbili,mfano; rais barack obama ni chotara kwa kuwa baba yake ni mjaluo wa kenya na mamae ni mtu wa ulaya,mulâtre kwa kifaransa.

5. FAKACHI ao FITNA: ni tabia ya mtu kusema mambo ya watu wengine ili kuwachochea,comérage kwa kifaransa.

6. RABA: viatu vyenye soli ya mpira.

7. SOLI: Sehemu ya chini ya kiatu unayotumia kwa kukanyagia unapotembea.

8. MZEE: Mtu mwenye umri mkubwa.

9. AJUZA (MAAJUZA wingi): Ni mzee wa kike.

10. SHAIBU: Mzee wa kiume.  

Mwisho wa kipindi.


Darasa-la-kiswahili