Divertissement: Amani Kwanza Band ya Eto Dunia kutoka Canada ya burudisha wa Tanzania

show time ETO Zibenga 
Bongo kuna mambo sana! Wasanii kibao wa kibongo Ijumaa usiku waliibukia katika bendi iliyojulikana kama Amani Kwanza iliyotambulisha albam yake ndani ya Mango Garden Kinondoni.
Bendi ikatajwa kuwa inatokea Canada huku asilimia 3 tu ya wasanii ndio wakiwa wanatokea Canada na asilimia zilizosalia ni wasanii wa hapa nyumbani. Miongoni mwa wasanii hao walikuwepo mwimbaji wa Double M Plus Dogo Rama na mwimbaji wa TOT Band Frank Kabatano.
Mpiga drum alikuwa ni Bally Tempo wa FM Academia huku bass likikung’utwa na Kilonzo msanii wa zamani wa Malaika Band.
Madansa wote walikuwa ni kutoka bendi mbalimbali za hapa nyumbani akiwemo Sabrina wa Akudo Impact. Wasanii halisi watatu wa Amani Kwanza Band waliongozwa na Eto Dunia na Luundo Dunia ambao walirekodi albam na wasanii hao wa kibongo na kuipa jina la “Pembe nne za Dunia”.

Msanii mwingine aliyeshiriki katika albam hiyo ni Totoo ze Bingwa wa BMM Band ambaye licha ya kutangazwa kuwa atakuwepo Mango Garden lakini hakutokea. Onyesho hilo lililosindikizwa na FM Academia na Jahazi Modern Taarab, lililalamikiwa na baadhi ya wadau wa muziki kutokana na kile kilichokuwa kikirudiwa mara kwa mara kuwa bendi ni Amani Kwanza kutoka Canada.
Wadau hao wakahoji iweje waambiwe kuwa bendi inatoka Canada wakati wasanii karibu wote ni watumishi wa bendi za hapa nyumbani na hawajasikia hata siku moja kuwa waliienda Canada. Uwepo wa msanii kama Dogo Rama ulileta mkanganyiko mkubwa hasa ukizingatia kuwa ni majuzi tu alitabulishwa katika ukumbi huo huo kama msanii mpya Double M Plus na mbaya zaidi ni kuwa hadi mashabiki wanaodoka ukumbini hawakuwekwa wazi iwapo wasanii hao wa kibongo walikuwepo kwaajili tu ya ‘project’ maalum.

Eto Dunia na Luundo Dunia ni wazaliwa wa Congo wanaoishi Canada lakini pia wakiwa wana uenyeji wa kutosha hapa Bongo.
Licha ya malalamiko hayo ya hapa na pale, mkusanyiko huo uliounda Amani Kwanza Band, ulishuka na mziki mzito uliosisimua mashabiki waliofika Mango Garden. Bado haijajulikana kama bendi hiyo itahamishia maskani yake Bongo na kusajiliwa BASATA au la.

 Frank Kabatano (kulia) akiwachezesha madansa wa Amani Kwanza
Frank Kabatano (kulia) akiwachezesha madansa wa Amani Kwanza
 Mambo hayo!!!
Mambo hayo!!!
 Kulia ni Dogo Rama ndani Amani Kwanza Band
Kulia ni Dogo Rama ndani Amani Kwanza Band
 Eto Dunia mwimbaji na bosi wa Amani Kwanza
Eto Dunia mwimbaji na bosi wa Amani Kwanza
Nyoshi el Saadat (kulia) akifuatilia onyesho la Amani Kwanza
Nyoshi el Saadat (kulia) akifuatilia onyesho la Amani Kwanza
 Mzee Yussuf akiimba katika onyesho la Amani Kwanza
Mzee Yussuf akiimba katika onyesho la Amani Kwanza
 Waimbaji wa Jahazi
Waimbaji wa Jahazi
Dj Bullah akiwa na Ali Yanga (kulia)
Dj Bullah akiwa na Ali Yanga (kulia)
Wadau wa muziki kutoka kushoto ni Ben Kaguo, Said Mdoe, Dj Bullah wa Clouds FM, Kiff Jr
Wadau wa muziki kutoka kushoto ni Ben Kaguo, Said Mdoe, Dj Bullah wa Clouds FM, Kiff Jr